Hati
ya Maandishi ya Ajira
Sheria ya kazi ya Tanzania inahitaji
kwamba wafanyakazi wapewe mkataba ulioandikwa wa ajira wanapoanza ajira
isipokuwa kwa wale ambao wanafanya kazi chini ya siku 6 kwa mwezi kwa mwajiri
fulani. Huenda mkataba wa ajira ukuwa wa kipindi chenye kikomo au kisichokuwa
na kikomo au kazi maalum. Lazima mkataba wa ajira uwe umeandikwa ukiwa unampa
mfanyakazi huyo kufanya kazi nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania.
Mkataba wa ajira lazima ueleze
maelezo yafuatayo. Jina, umri, anwani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali
pa kuajiriwa; ufafanuzi wa kazi; tarehe ya kuanza; aina na muda wa mkataba;
mahali pa kazi; saa za kufanya kazi; ujira, mbinu ya hesabu yake, na maelezo ya
faida aiu malipo ya aina yoyote, na suala lingine lililofafanuliwa. Hata hivyo,
ikiwa vipengele hivi vimetolewa tayari katika mkataba wa ajira, huenda mwajiri
asijaze hali iliyoandikwa ya vipengele vya ajira.
Lazima mwajiri ahakikishe kwamba
vipengele vyote vilivyoandikwa vimefafanuliwa wazi kwa mfanyakazi kwa njia
inayoeleweka na mfanyakazi. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika kipengele
chochote kilichoandikwa, mwajiri anahitajika kupitia upya vipengele
vilivyoandikwa kwa kushauriana na mfanyakazi ili kuangazia mabadiliko hayo.
Lazima mwajiri amfahamishe mfanyakazi kuhusu mabadiliko hayo kwa kuandika.
Mwajiri anawajibika kuweka vipengele
vilivyoandikwa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya ajira kuisha. Ikiwa
mwajiri atashindwa kutoa mkataba ulioandikwa katika kesi zozote za kisheria,
mzigo wa kuthibitisha au kukataa masharti fulani ya ajira uko kwa mwajiri. Kila
mwajiri lazima aonyeshe taarifa ya haki ya wafanyakazi katika mahali
panapoonekana.
Chanzo: Sehemu ya 14-16 ya Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004.
Mkataba
wa kazi wa kipindi maalumu
Kwa mujibu wa sheria za kazi za
Tanzania, ni marufuku kuajiri mfanyakazi kwa kipindi cha muda maalumu uliotajwa
kwa kazi zenye asili ya kudumu. Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina kati ya
zifuatazo-(a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; mkataba kwa kipindi cha
muda kilichotajwa kwa kazi za wataalamu na mameneja, mkataba wa kazi maalumu.
Hakuna sehemu yeyote kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004
inayotoa maelezo juu ya kuendeleza mkataba au muda wa juu wa mkataba wa kipindi
maalumu.
Ikiwa mfanyakazi ataendelea
kufanyakazi baada ya kipindi maalum kuisha, haki na majukumu hubaki sawa, bila
kuwa kwa makubaliano yoyote yanayopinga, kama yalivyokuwa mwisho wa kipindi.
Ikiwa hakuna muda maalum wa ushirikiano, mwezi yeyote anaweza kubainisha
ushirkiano wakati wwote baada ya kutoa ilani ya lengo lake kwa wenza wale
wengine.
Chanzo: Sehemu ya 14 ya Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004. Sehemu ya 197 na 200 ya Sheria za Mkataba
Kifungu cha 345
Kipindi
cha majaribio kazini
Sheria za kazi katika Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 hazisemi wazi ni kwa muda gani mfanyakazi
atakuwa katika majaribio kazini chini ya mwajiri wake. Hata hivyo, sheria hii
inatamka japo si wazi sana kwamba Mafanyakazi mwenye chini ya miezi 6 kazini
iwapo ataachishwa kazi hawezi kulalamika kuwa ameachishwa kwa hila.
Chanzo: Sehemu ya 35 ya Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004
Taratibu/mwongozo
wa hali za ajira
- Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
- Sheria ya sikukuu za kitaifa, 1966 / Public Holidays Ordinance, 1966
Kuhusiana
mada
No comments:
Post a Comment