Tuesday, 6 December 2016

Vyombo vya mawasiliano

Namna ya kuandika barua


Masatu Sobago

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Unapoondika Barua ya Kuomba Kazi
Barua ya kuomba kazi ni waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika kuomba kazi. Ni vyema barua ya kuomba kazi ikaandaliwa kwa umakini, na kujaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi kumvutia mwajiri mtarajiwa.
Kwa kuzingatia kanuni za kawaida za kuandika barua rasmi za kiofisi, kama mahali inapokuwepo anuani ya mwandikaji, mwandikiwa, tarehe, saini, na kadhalika, mambo yafuatayo ni muhimu kutiliwa mkazo unapoandika barua ya kuomba kazi/ajira:
1. Kichwa cha habari (barua) kinachoeleweka
Hakikisha kichwa cha habari kinajitosheleza. Tumia maneno yanayotaja nafasi husika inayoombwa wazi wazi ili kumsaidia msomaji kujua unataka nini. Ni muhimu kutumia maneno yaliyo wazi na yanayoeleweka kwa urahisi kwa kuelewa kwamba mpokea maombi wakati mwingine hana muda wakufikiria ulichoandika.
Mfano,
'YAH: KUOMBA KAZI YA MHASIBU MSAIDIZI KATIKA KAMPUNI YAKO...'
Hapo inafahamika unataka nini moja kwa moja.
2. Onesha ulikopata habari za kazi unayoomba
Baada ya kuridhika na kichwa cha habari, ni muhimu sentesi inayoanza chini yake, kurejea tarehe ya tangazo la kazi unayoomba pamoja na namba ya kumbukumbu kama ipo au eleza ulivyosikia kuwepo kwa nafasi ya kazi.
Mfano, " Rejea tangazo lako la nafasi ya kazi lenye kumbukumbu namba XXX katika gazeti la Mtanzania la tarehe 24 Agosti 2014."
Wengine wanapenda kuandika sentensi zisizo za lazima kama, "Kichwa habari hapo juu chakusika" . Ni mazoea tu lakini hulazimiki kuanza namna hiyo.
3. Sema wazi unaomba kazi
Baada ya kusema ulikopata habari za kazi unayoomba, tumia sentensi inayofuata kueleza nia yako ya kuomba kazi hiyo. Kumbuka msomaji wa barua hana muda wa kusoma maelezo yako mengi, ni muhimu kuandika kila kitu kwa kifupi na kwa uwazi.
Mfano, " Ninaandika barua hii kuomba kazi ya Uhasibu katika kampuni/shirika/taasisi yako kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo nililolitaja."
4. Oanisha majukumu ya kazi na ujuzi ulionao
Kinachofuata katika aya zinazofuata ni kuonyesha namna unavyoweza kumudu majukumu yaliyotajwa kwenye tangazo hilo kwa kuyaoanisha na ujuzi na sifa za kitaaluma ulizonazo pamoja na uzoefu wa kazi ulionao. Mara nyingi majukumu ya kazi huainishwa katika tangazo la kazi hivyo ni muhimu sana kuonesha unavyokidhi majukumu hayo moja kwa moja.
Kama majukumu hayo hayajaonyeshwa kwenye tangazo la kazi, ni vyema kufanya utafiti kujua majukumu hayo. Mwajiri anategemea utafanya uchunguzi vizuri kabla hujaandika barua.
Mfano, " Ninao uwezo wa kutunza kumbukumbu sahihi za mahesabu ya kampuni yako, kwa sababu, mbali ya kusomea Cheti cha Uhasibu katika Chuo cha Uhasibu Buguruni, nina uzoefu wa kujitolea kwa miezi 13 nikifanya kazi za uhasibu katika Kampuni XXX. Kadhalika, nimepata mafunzo ya kutunza fedha kwa njia ya mtandao hivyo ninaweza kumudu majukumu hayo ipasavyo. "
5. Hitimisha kwa uungwana na ufasaha
Ni vyema kuhitimisha barua yako kwa kuonesha unavyofaa kwa kazi unayoiomba. Uchaguzi makini wa maneno kutakupa alama za ziada kuonyesha kwamba unajua kuwasiliana vizuri. Hakuna mwajiri angependa kuajiri mtu asiyejua kujieleza ipasavyo.
Mfano, unaweza kusema unatanguliza shukrani zako za dhati na kueleza kwamba uko tayari kuitwa kwa usaili. Unaweza kumaliza kwa kutaja nyaraka ulizoambatanisha pamoja na barua hiyo.
Mambo ya kuepuka
Unapoandika barua muhimu kama ya kazi, tumia maneno yanayojenga taswira ya mtu aliyetulia, mwenye heshima na uelewa, anayeweza kuuelezea uwezo wake vizuri bila kuonyesha majivuno yasiyo na sababu. Epuka kutumia maneno ya amri, yasiyoonesha unyenyekevu, maneno ya mtaani yasiyo rasmi.
Huna sababu ya kutaja jina la mwenye kupokea maombi hayo hata kama unamfahamu. Taja cheo chake ikiwa ni lazima, lakini kutumia maneno kama Ndugu, Dear Sir/Madam ni muafaka zaidi.
Kadhalika, hakikisha lugha unayotumia ni fasaha, inaeleweka na haina makosa ya kiuandishi. Epuka makosa makosa ya kisarufi yanatoa picha ya uzembe na uvivu na yanaweza kukugharimu hata kama ni kweli sifa za kitaaluma unazo. Kumbuka, si sifa za kitaaluma pekee hutumika kufanya maamuzi ya kuajiri ama kutokuajiri.
Aidha, huna haja ya kujitambulisha na kutoa taarifa zisizo za lazima na ambazo ulizitaja kwenye wasifu utakaouambatanisha.
Kwa mfano, haifai kujaza karatasi kwa maelezo kama, "Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 24 nilizaliwa kwenye kijiji cha Kwa Mtoro Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma. Nimesoma shule ya Chekechea wilayani Rorya, na kisha nikahamia Kyela kwa masomo ya Shule ya Msingi mpaka darasa la pili kisha...nikahamia shule ya msingi Lomwe, kisha nikaenda....na kadhalika ". Maelezo haya yanakatisha tamaa, na yanaonyesha huna ubunifu wala mbinu za kuwasiliana.
Mwisho na muhimu, ni makosa ya kujitakia kushawishika kutoa taarifa za uongo katika jitihada za kutaka kujenga taswira chanya isiyokuwepo. Sifa usizostahili, achana nazo. Zitakugharimu.
Kwa kuhitimisha, barua ya maombi ya kazi ni jaribio lako kwa mwajiri kuonyesha namna ulivyo mbunifu na mwenye uwezo wa kuwasiliana ipasavyo. Itumie fursa hiyo uwezavyo.
Ni jambo la busara kuelewa kwamba kuomba kazi si kupata kazi. Ni sehemu ya safari ambayo wakati mwingine huchukua muda mrefu kupata majibu yakufurahisha. Wakati unaposubiri majibu, ni busara kufanya shughuli zinazoweza kukukuza na kukuendeleza kiujuzi hata ikibidi kwa kujitolea pasipo ujira.
Mwandishi wa makala haya ni Mhadhiri Msaidizi wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Anapatikana kwa barua pepe: bwaya@mwecau.ac.tz
Twitter: @bwaya
Una kazi ya kuoanisha majukumu ya kazi unayoomba na sifa lulizonazo. PICHA @Ongeza maoni

Wednesday, 30 November 2016

Usalama wa Ajira



Hati ya Maandishi ya Ajira
Sheria ya kazi ya Tanzania inahitaji kwamba wafanyakazi wapewe mkataba ulioandikwa wa ajira wanapoanza ajira isipokuwa kwa wale ambao wanafanya kazi chini ya siku 6 kwa mwezi kwa mwajiri fulani. Huenda mkataba wa ajira ukuwa wa kipindi chenye kikomo au kisichokuwa na kikomo au kazi maalum. Lazima mkataba wa ajira uwe umeandikwa ukiwa unampa mfanyakazi huyo kufanya kazi nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania.
Mkataba wa ajira lazima ueleze maelezo yafuatayo. Jina, umri, anwani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali pa kuajiriwa; ufafanuzi wa kazi; tarehe ya kuanza; aina na muda wa mkataba; mahali pa kazi; saa za kufanya kazi; ujira, mbinu ya hesabu yake, na maelezo ya faida aiu malipo ya aina yoyote, na suala lingine lililofafanuliwa. Hata hivyo, ikiwa vipengele hivi vimetolewa tayari katika mkataba wa ajira, huenda mwajiri asijaze hali iliyoandikwa ya vipengele vya ajira.
Lazima mwajiri ahakikishe kwamba vipengele vyote vilivyoandikwa vimefafanuliwa wazi kwa mfanyakazi kwa njia inayoeleweka na mfanyakazi. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika kipengele chochote kilichoandikwa, mwajiri anahitajika kupitia upya vipengele vilivyoandikwa kwa kushauriana na mfanyakazi ili kuangazia mabadiliko hayo. Lazima mwajiri amfahamishe mfanyakazi kuhusu mabadiliko hayo kwa kuandika.
Mwajiri anawajibika kuweka vipengele vilivyoandikwa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya ajira kuisha. Ikiwa mwajiri atashindwa kutoa mkataba ulioandikwa katika kesi zozote za kisheria, mzigo wa kuthibitisha au kukataa masharti fulani ya ajira uko kwa mwajiri. Kila mwajiri lazima aonyeshe taarifa ya haki ya wafanyakazi katika mahali panapoonekana.
Chanzo: Sehemu ya 14-16 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004.
Mkataba wa kazi wa kipindi maalumu
Kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania, ni marufuku kuajiri mfanyakazi kwa kipindi cha muda maalumu uliotajwa kwa kazi zenye asili ya kudumu. Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina kati ya zifuatazo-(a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kazi za wataalamu na mameneja, mkataba wa kazi maalumu. Hakuna sehemu yeyote kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004 inayotoa maelezo juu ya kuendeleza mkataba au muda wa juu wa mkataba wa kipindi maalumu.
Ikiwa mfanyakazi ataendelea kufanyakazi baada ya kipindi maalum kuisha, haki na majukumu hubaki sawa, bila kuwa kwa makubaliano yoyote yanayopinga, kama yalivyokuwa mwisho wa kipindi. Ikiwa hakuna muda maalum wa ushirikiano, mwezi yeyote anaweza kubainisha ushirkiano wakati wwote baada ya kutoa ilani ya lengo lake kwa wenza wale wengine.
Chanzo: Sehemu ya 14 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004. Sehemu ya 197 na 200 ya Sheria za Mkataba Kifungu cha 345
Kipindi cha majaribio kazini
Sheria za kazi katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 hazisemi wazi ni kwa muda gani mfanyakazi atakuwa katika majaribio kazini chini ya mwajiri wake. Hata hivyo, sheria hii inatamka japo si wazi sana kwamba Mafanyakazi mwenye chini ya miezi 6 kazini iwapo ataachishwa kazi hawezi kulalamika kuwa ameachishwa kwa hila.
Chanzo: Sehemu ya 35 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004
Taratibu/mwongozo wa hali za ajira
  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Sheria ya sikukuu za kitaifa, 1966 / Public Holidays Ordinance, 1966
Kuhusiana mada

Sunday, 20 November 2016

matangazo ya msp




]
MASATU SERVICE PROVIDER
S.L.P ……...  BUNDA
0684112154/0752678604
INAPENDA KUWATANGAZIA HUDUMA MBALIMBALI TUNAZOTOA KAMA IFUATAVYO:-
MASATU SERVICE PROVIDER
Ø KUCHAPISHA MAPACHISHO YOTE
Ø KUTENGENEZA KADI ZA HARUSI,VIKUNDI ,MWALIKO,MICHANGO & DESIGNING
Ø KUTENGENEZA VYETI VYA MATUKIO MBALIMBALI ( CERTIFICATE DESIGNING)
Ø KUPIGA PICHA AINA YA ZOTE ( PASSPORT SIZE EXPRESS) NA KUSAFISHA
Ø HUDUMA ZA KURUDUFU AU KUANDIKA MAANDISHI AINA ZOTE ( HUDUMA YA PHOTOCOPY & PRINTING)
Ø SCANNING
Ø TUNACHOMA NYIMBO KWENYE CDR / DVDR, MEMORY CARD & FLASH
Ø TUNAUZA HOUSING ZA SIMU,BETRI ZA  SIMU, FLASH, CDR / DVDR, MEMORY CARD & KADIRIDER ZA MEMORY
Ø HUDUMA YA ODERING YA KIFAA/KITU CHOCHOTE


KARIBUNI SANA TUPO CHITARE CENTER

Saturday, 19 November 2016

MAWASILIANO


KWA LOLOTE USISITE KUWASILIANA NASI

Email:masatusobago23@gmail.com
Tell:0752678604
0684112154
0627619981
0676175594